Wednesday, March 13, 2013

Makosa makubwa katika video ya Lwakatare


MAPUNGUFU YA VIDEO ILIYOBEBA UMAARUFU KUHUSU LWAKATARE KUHUSIKA NA MIKAKATI YA MAUAJI.......WENYE UELEWA KARIBUNI 

1. video imechukuliwa tarehe 28-12-2012 baada ya sikukuu ya krismasi bila shaka kama tulivyowasikia wahusika humo. kwanini video ije kutolewa saiv baada ya tukio la kuteswa ?


2. hii video imechukuliwa na camera yenye MEGA PIXEL zaidi ya 5, na secret cameras huwa hazina pixel kubwa kiasi hicho. hivyo wahusika walikua wanajua kabisa kuwa wanajirekodi..

...
3. kauli ya ridhiwan na nape kuhusu kuwa wanayo video ikiwaonesha viongozi wa chadema wakipanga mauaji ya watu, tangu chadema iseme pelekeni hiyo video kwenye vyombo vya dola hili wahusika wachukuliwe hatua ccm hawakupeleka inamaana hii video ilikua bado au ? na ikumbukwe hii video imechukuliwa 28-12-2012 na mwigulu alisema wanazo video ni tarehe hizo hizo.

4. mhusika kuweka hiyo video "BUKOBA BOY" amejiunga na youtube tarehe 11-03-2013, na tarehe hiyo hiyo akaweka hiyo video ambayo aliichukua tarehe 28-12-2012, je kama analipenda taifa hili kwanini hasingeweka tangu kabla ya tukio pengine kibanda angeepukana na hatari hii..?


5. kama kweli polisi inanguvu kwanini haijamkamata huyu mtu mpaka saiv kwakua ni threat kwa taifa ?


6. katika dakika ya 16 na sekunde ya 55 ya video hii, lwakatare anasema" either nilivyopewa na kuistudy hii homework" inamaana kuna mtu kamtuma kusema haya maneno ? swali je ni nani ?


7. katika dakika ya 17 sekunde ya 32 lwakatare anasema" kama huyu mtu anakua na sehemu nyingi sasa tutatrace ngapi, lazima hawe na sehemu moja specific kuwa hakosi" jamani tujuzane hivi mtu anaepanga mauaji anachagua sehemu kweli ? mbona mwangosi aliuliwa kwenye mikono ya polisi inamaana huwa ndio ilikua sehemu yake ? mbona kijana kwenye maandamano alikufa kwenye mkutano inamaana morogoro kila siku palikua na mikutano na marehemu alikua ndio sehemu yake ?


8 na mwisho kwanini video imekatiswa katikati ? je kuna matukio mengine yatafanyika alaf ndio waje na video ya 6 maana hiyo ni video ya 5 ?


9. mwanzo kabisa ya video wanarekebisha mic, na mchukua video anasema "tuta-note upya hapo" inamaana kuna marekebisho ya kubadiri camera yalifanyika hata video inavyoanza tunaona kabisa walikua kimya.


hayo ni baadhi ya mapungufu niliyoyaona humo